Thursday, May 16, 2013

SIKU MIA ZA MGOMO WA CHAKULA GUANTANAMO


Huku zikiwa zimewadia siku 100 tokea wafungwa waanze mgomo wa chakula katika gereza ya kuogofya ya Guantanamo Bay inayosimamiwa na jeshi la Marekani, waliowengi duniani wanataka haki za wafungwa hao ziheshimiwe na gereza hiyo ifungwe..
Mawakili wa wafungwa wa Guantanamo wanasema idadi ya waliokatika mgomo wa chakula ni zaidi ya 100 ambao wametangazwa rasmi. Kuna wafungwa 166 katika gereza hiyo. Hivi sasa wafungwa 30 waliogoma kula wanalishwa kwa nguvu kupitia mrija puani. Mkenya pekee anashikiliwa  Guantanamo, Abdulmalik Mohammad, amejiunga na wafungwa wenzaka ambapo wamesusia chakula kama njia ya kulalamikia kuendelea kushikiliwa pasinda kufunguliwa mashtaka.
Wafungwa hao katika jela hiyo ya kutisha walianza mgomo wa kutokula chakula tangu mwezi Februari mwaka huu wakilalamikia hali mbaya ya jela hiyo, kuporwa vitu vyao zikiwemo barua, kuwadhalilisha na kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu, hususan nakala za Qur’ani Tukufu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO