Upinzani nchini Syria leo umeitaka jumuiya ya kimataifa kuweka eneo la kupitisha misaada ya kiutu kusaidia watu walioko katika mji wa Qusayr, ambako mapigano makali kati ya majeshi ya serikali na waasi yanaendelea. Kaimu mkuu wa baraza la muungano wa kitaifa George Sabra amesema kuwa anaitaka jumuiya ya kimataifa kuweka eneo ambalo litatumika kuwasaidia watu waliojeruhiwa na kuingiza madawa na misaada mingine kwa watu zaidi ya 50,000 ambao wamezingirwa. Amewataka pia waasi nchini humo kwenda haraka huko ili kuudhibiti tena mji wa Qusayr , mji ambao unaendelea kushambuliwa na majeshi ya serikali yakisaidiwa na wapiganaji wa kundi la Hezboullah kutoka Lebanon.
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ya Kiarabu Ahmad Ben Helli amesema mataifa hayo yameshutumu kile kichotokea Qusayr. Wakati huo huo naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Syria Faisal Muqdad anatarajiwa kuwasili mjini Moscow leo kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov kuhusiana na mkutano unaopangwa kumaliza mzozo nchini Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO