Mkuu wa majeshi ya Israel ameionya serikali ya rais Bashar al-Assad kwamba itachukuliwa hatua iwapo mashambulio ya risasi yataendelea kutoka katika eneo la Syria dhidi ya majeshi ya Israel katika eneo linalokaliwa na nchi hiyo la milima ya Golan. Luteni jenerali Benny Gantz amesema katika televisheni ya Israel kuwa hataruhusu milima ya Golan kuwa eneo rahisi kwa al-Assad. Amezungumza saa chache baada ya majeshi ya Israel kufyetuliana risasi katika eneo lililotengwa kusitisha mapigano la milima ya Golan, lakini taifa hilo la Kiyahudi limekana madai ya Syria kuwa gari lake moja la kijeshi limeharibiwa. Syria inadai kuharibu gari hiyo ya kijeshi ya Israel ambayo inasema ilivuka eneo la kusitisha mapigano wakati wa tukio hilo. Siku ya Jumatatu jeshi liliripoti kuwa mashambulio ya silaha ndogo ndogo kutoka upande wa Syria yalifika katika eneo linalodhibitiwa na Israel la milima ya Golan, lakini hakuna athari yoyote iliyotokea.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO