Waziri Mkuu wa Uturuki, Tayipp Erdogan, amesema atauzuia mpango wa ujenzi kwenye Bustani ya Gezi. Hapo jana, Erdogan alikutana na kundi la upinzani la Mshikamano wa Taksim kujadiliana namna ya kumaliza machafuko. Kundi hilo lililopewa jina la uwanja uliofungwa kwenye Bustani hiyo ya Gezi, lilisema Erdogan atangojea uamuzi wa mahakama, juu ya mpango wake wa ujenzi, na kwamba ataitisha kura ya maoni ikiwa uamuzi wa mahakama utaipendelea serikali. Ukandamizaji dhidi ya maandamano ya amani kwenye bustani hiyo wiki mbili zilizopita ulichochea maandamano dhidi ya kiongozi huyo wa Uturuki, na chama chake cha Haki na Maendeleo. Takribani kila siku ndani ya wiki hizo mbili polisi walitumia gesi za machozi na magari ya maji yanayowasha dhidi ya waandamanaji.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO