Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais wa Iran yanaonesha kuwa ulamaa mwenye msimamo wa wastani, Hassan Rowhani, anaongoza. Kwa mujibu wa tangazo la wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo, kati ya kura zaidi ya 800,000 kutoka zaidi ya vituo 1,600, Rowhani amejizolea zaidi ya nusu, huku mpinzani wake wa karibu, Meya wa Tehran, Mohammad Baqer Qalibaf, akipata kura 126,000. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mohammad Najjar, amesema kuwa kiwango kikubwa cha watu waliojitokeza kupiga kura kimechelewesha kazi ya kuhisabu kura. Wagombea wote sita wanaonekana kuwa wahafidhina, ingawa Rowhani alijaribu kuwavutia wanamageuzi katika kampeni zake. Matokeo kamili yanatarajiwa kupatikana hapo kesho.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO