Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kuiunga mkono Syria ni kuunga mkono mapambano dhidi ya utawala bandia wa Israel.
Sheikh Naim Qasim amesema Hizbullah haina lengo jingine ghairi ya kudumisha muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati na kukabiliana na chokochoko za Israel sambamba na kukata mikono ya magaidi. Akiashiria kwamba, harakati hiyo haina nia nyingine katika vita vya Syria zaidi ya muqawama amefafanua kuwa, wapiganaji wa Hizbullah wamesimama imara kukabiliana na waitifaki wa Marekani, Israel na makundi ya kigaidi katika eneo hili.
Sheikh Naim Qasim amesisitizia udharura wa kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za kisiasa na maelewano kati ya makundi yote hasimu ili kwa njia hiyo waweze kuvunja njama za maadui wa taifa hilo la Kiarabu. Amesema matukio ya Syria yanajiri chini ya njama dhidi ya Lebanon na eneo kwa ajili ya kuanzishwa Mashariki ya Kati mpya kwa manufaa ya Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO