Nchi za Kiarabu zilizoko katika eneo la Ghuba ya Uajemi zimeendeleza uadui dhidi ya Mashia wa Lebanon, baada ya serikali ya Qatar kuwafukuza nchini humo raia 17 wa Lebanon kwa tuhuma wanashirikiana na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon. Taarifa zinasema kuwa, serikali za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu nazo hivi karibuni zilitangaza kuwafukuza raia kadhaa wa Lebanon kwa tuhuma za kushirikiana na harakati ya Hizbullah. Televisheni ya Qatar imeeleza kuwa, harakati ya Hizbullah ilikuwa na nafasi kubwa katika shambulio lililofanywa na majeshi ya Syria na hatimaye kuukomboa mji wa kiistratijia wa Qusayr mwanzoni mwa mwezi huu. Hii ni katika hali ambayo, serikali za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi zimekuwa zikishindwa kuficha hasira na chuki zao dhidi ya mafanikio ya wapiganaji wa Hizbullah katika mapambano yao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO