Saturday, June 01, 2013

ICC YATUPILIA MBALI TAKWA LA LIBYA

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imetupilia mbali takwa la serikali ya Libya la kutaka usimamishwe mpango wa kumtia mbaroni Seiful Islam Gaddafi mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu wakati wa kukaribia kuangushwa utawala wa baba yake mwaka 2011. Taarifa ya mahakama hiyo iliyoko The Hague nchini Uholanzi imeeleza kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliipatia mahakama hiyo jukumu la kuchunguza mgogoro wa Libya na hatimaye kutoa waranti wa kutiwa mbaroni  Kanali Muammar Gaddafi kabla ya kuuawa, Seiful Islam Gaddafi na Abdullah Sanusi mkuu wa zamani wa shirika la kiintelijinsia la Libya mwaka 2011.  Hii ni katika hali ambayo Mahakama ya ICC na serikali ya Libya zinahitilafiana kimitazamo juu ya mahali atakapohukumiwa Seiful Islam, ambaye alitiwa mbaroni na wafanya mapinduzi mwezi Novemba 2011.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO