Mkuu wa zamani wa chama cha Al-Kata'ib nchini Lebanon, amesema kuwa, baadhi ya nchi za eneo ikiwemo Qatar, zinapanga njama ya kuligeuza eneo la mji wa Tripoli nchini humo, kuwa ngome ya kundi la kigaidi la Al-Qaida. Karim Baqraduni ameyasema hayo alipozungumza na Shirika la Habari la Fars News na kuongeza kuwa, katika hali ambayo wananchi wengi wa mji wa Tripoli, Lebanon wanasisitizia juu ya usalama na amani, amma kundi dogo la Jab'hatu Nasra na Al-Qaida yanafanya njama kwa ajili ya kuzusha fitina na kuufanya mji huo kuwa eneo lao la kutekelezea vitendo vya ugaidi. Karim ameongeza kuwa, wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida unaopata himaya kutoka kwa Qatar na Marekani, wanafanya njama hizo kwa maslahi ya utawala haramu wa Kizayuni. Kabla ya hapo Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Chama cha Demokratic nchini Lebanon Raf'at Idd alikosoa mwenendo wa kisiasa wa serikali ya Bairut kwa kushindwa kukabiliana na machafuko mjini Tripoli na kusema kuwa, ikiwa mgogoro huo hautamalizika, basi kuna hatari ya kuenea katika maeneo yote ya Lebanon. Karibu watu 30 wameripotiwa kuuawa katika machafuko ya wiki iliyopita katika maeneo ya Bab al-Tabbaneh na Jabal-Mohsenya mjini Tripoli.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO