Maelfu ya wapinzani na waungaji mkono wa Rais Muhammad Morsi wamefanya maandamano mjini Cairo, Misri. Taarifa zinasema kuwa, wanaharakati wa kisiasa wa makundi ya Kisalafi na baadhi ya makundi yenye misimamo ya Kiislamu inayokaribiana na harakati ya Ikhwanul Muslimiin yamefanya maandamano ya kuunga mkono maamuzi yaliyochukuliwa hivi karibuni na Rais Morsi wa nchi hiyo. Waandamanaji hao walikusanyika mkabala wa Masjidul Rabi'i al A'dawiya mjini Cairo, na kutaka itekelezwe sheria za Kiislamu nchini humo.
Kwa upande mwingine, wapinzani wa Rais Morsi walikusanyika mkabala wa Wizara ya Ulinzi wakilalamikia maamuzi yaliyochukuliwa hivi karibuni na kiongozi wa nchi hiyo. Duru mpya ya maandamano nchini Misri imeshuhudiwa baada ya Rais Morsi kufanya mabadiliko ya Magavana wa majimbo kadhaa nchini humo. Wapinzani wanadai kwamba shakhsia wengi wa Kisalafi na Ikhwanul Muslimin wamepewa nyadhifa muhimu nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO