Sunday, June 16, 2013

WAISLAM UK KUSUSIA TENDE ZINAZOTOKA ISRAEL

Jamii ya Waislamu nchini Uingereza inapanga kuanzisha kampeni maalumu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani dhidi ya vitongoji vya utawala wa Kizayuni wa Israel vinavyojengwa katika ardhi za Wapalestina. Kampeni hiyo ni ya kuwashajiisha Waislamu wa nchi hiyo wasusie kununua tende za Israel zinazolimwa katika ardhi za Palestina zilizojengwa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Ufukwe wa Magharibi na katika bonde la Jordan. Karibu nusu ya walowezi wa Kizayuni waishio kwenye bonde la Jordan ni wakulima wa tende, zao ambao ndilo linalochangia sehemu kubwa ya pato lao la uchumi. Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza (MAB) imeeleza kuwa itatangaza siku ya taifa ya uchukuaji hatua dhidi ya sera za ujenzi wa vitongoji ya Israel. Kampeni dhidi ya sera hiyo ya utawala wa Kizayuni itakayoanza tarehe 21 mwezi huu yaani takribani wiki mbili kabla ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani inaungwa mkono na jumuiya zaidi ya 20 ikiwemo ya Marafiki wa Al-Aqsa na ya Kampeni ya Mshikamano na Palestina ambazo ndizo jumuiya mbili kubwa zaidi zinazoipinga Israel nchini Uingereza na barani Ulaya kwa ujumla. Israel inazalisha kiwango kikubwa cha tende aina ya Medjool zinazolimwa kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina katika Ufukwe wa Magharibi na bonde la Jordan. Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza (MAB) imesisitiza kuwa kununua tende hizo kutakuwa na maana ya Waislamu kutumia fedha zao kuunga mkono wizi wa ardhi ya Palestina na ukandamizaji dhidi ya Wapalestina. Ripoti zinaeleza kuwa katika mwaka 2011 utawala wa Kizayuni wa Israel ulipata faida ya dola milioni 265 kutokana na uuzaji wa tende za Medjool

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO