Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi msaada zaidi kutoka kwa serikali kwa waathiriwa wa mafuriko mashariki mwa Ujerumani.Hapo jana Merkel aliwasifu maelfu ya watu ambao wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kukabiliana na athari za mafuriko.Kiasi ya watu 40,000 wamelazimika kuhama makwao.Merkel aliwaambia wahisani huko Wittenberge katika ukingo wa mto Elbe waliokuwa wakijaza magunia mchanga kuwa wajerumani wanapaswa kujivunia kwa kuungana wakati wa hali ngumu.Kiasi ya wazima moto 70,000 na wanajeshi 11,000 pamoja na raia waliojitolea wanasaidia kukabiliana na athari za mafuriko.Merkel amesema atajadili na viongozi wa majimbo 16 ya Ujerumani kuhusu kutolewa kwa misaada kwa waathiriwa katika mkutano utakaofanyika Alhamisi hii.Wiki kadhaa za kunyesha kwa mvua kubwa ulaya ya kati kumesababisha mito mikuu kuvunja kingo zake na kusababisha maafa makubwa kusini na kati mwa Ujerumani,katika Jamhuri ya Czech,Austria,Slovakia na Hungary.Kiasi ya watu 22 wameripotiwa kufariki.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO