Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini, ameiomba Sudan itatuematatizo yalipo kati ya Juba na Khartoum kwa njia ya mazungumzo ikiwa ni katika radiamali ya Rais huyo wa Sudan Kusini kufuatia hatua ya Sudan ya kutangaza kusimamaisha usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba ya nchi hiyo. Kiir amewaambia waandishi wa habari mjini Juba kuwa, nchi yake bado inapendekeza mazungumzo na Sudan kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza tofauti zilizopo kati ya nchi mbili. Ameongeza kuwa, kuna sababu za pamoja zinazozilazimu nchi mbili hizo kukaa chini na kutafakari njia ya kutatua suutafahumu kati yao. Kwa upande mwingine Rais Salvakiir wa Sudan Kusini, amelaani hatua ya kusimamishwa makubaliano yaliyofikiwa na nchi hizo mbili. Aidha amekadhibisha tuhuma zilizotolewa na Sudan kwamba nchi yake inayaunga mkono makundi ya waasi wanaoendesha vita dhidi ya serikali ya Khartoum na kusema kuwa, tuhuma hizo hazina ukweli wowote. Siku chache zilizopita Rais Omar Hassan Al-Bashir wa Sudan alitoa amri ya kusimamishwa usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kupitia bandari za nchi yake kutokana na serikali ya Juba kuwaunga mkono waasi wa Sudan.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO