Tuesday, June 11, 2013

MISRI HAITAKUBALI UJENZI WA BWAWA NCHINI ETHIOPIA

Rais Muhammad Mursi wa Misri ametangaza kuwa, nchi yake inayachunguza mapendekezo yote kuhusiana na mpango wa Ethiopia wa kujenga bwawa la an Nahdha, suala ambalo limeitia wasi wasi mkubwa serikali ya Cairo. Mursi aliyasema hayo hapo jana  na kusisitiza kuwa, nchi yake haitakubaliana kamwe na mpango huo. Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita, washauri wa rais huyo wa Misri waliitaka serikali ya Addis Ababa kusimamisha mara moja mpango wake wa kujenga bwawa la an Nahdha litakalotumia maji ya Mto Nile. Hii ni katika hali ambayo kabla ya hapo pia Waziri Mkuu wa Misri Hisham Qandil na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Muhammad Kamil Amr walikuwa wamesema kuwa wataelekea nchini Ethiopia kwa ajili ya kuwasilisha msimamo wa Cairo kuhusiana na suala hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO