Jeshi la Misri limetangaza kuwa, tofauti zilizopo kati ya nchi hiyo na Ethiopia hasa kuhusiana na ujenzi wa bwawa la an Nahdha la Ethiopia kwa kutumia maji ya Mto Nile, si mzozo wa kijeshi wa kuzifanya nchi hizo mbili kuingia vitani. Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Misri Kamanda Ahmad Ali na kuongeza kuwa, hivi sasa ni mapema mno kutaka mgogoro wa ujenzi wa bwawa la an Nahdha la nchini Ethiopia utatuliwe kwa njia za kijeshi. Wakati huo huo, viongozi wa Misri wametangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia kukaribia tarehe 30 ya mwezi huu ambapo imepangwa kufanyika maandamano makubwa ya kutaka kuishinikiza serikali ya Cairo kuitisha uchaguzi wa rais wa kabla ya wakati wake. Viongozi hao wamesema hatua hiyo ina lengo la kulinda usalama na amani ya nchi dhidi ya hatua yoyote ya uharibifu. Waziri wa Ulinzi wa Misri, Abdul Fatah Khalil As Sisi amesisitiza kuwa, jeshi la nchi hiyo, limejiandaa kikamilifu kulinda usalama wa wananchi na wa taifa kutokana na vitisho vyovyote vinavyoweza kutokea.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO