Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri, kimetoa tamko la maulama wa kidini akiwemo Yusuf Qardhawi, Mkuu wa Umoja wa Maulama wa Kiislamu, kikipinga wito wa kile kinachosemwa eti ni jihadi nchini Syria. Kauli hiyo imetolewa katika kikao cha maulama wa kidini kilichofanyika mjini Cairo hii leo. Sheikh Ali Shams mmoja wa maulama wa al Azhar amesema kuwa, chuo hicho hakijawahi kuunga mkono wito wa eti jihadi nchini Syria na pia hakijawahi kutia saini suala hilo. Hii ni katika hali ambayo awali baadhi ya watu akiwemo, Muhammad al-Arifi na Qaradhawi, walitoa fatwa zinazokwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu za kuhalalisha mauaji dhidi ya Waislamu chini ya mwamvuli wa kile walichosema kuwa, eti ni jihadi nchini Syria. Mgogoro wa Syria unazidi kuchukua sura mpya huku siku hadi siku Waislamu duniani wanazidi kufahamu hatari ya fitina mbaya ya kimadhehebu inayochochewa na Marekani, utawala haramu wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya serikali halali ya Damascus ambayo ni mbeba bendera ya muqawama na mapambano dhidi ya Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO