Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa China Xi Jinping wamekamilisha jana mazungumzo yao ya siku mbili yaliyolenga katika kile Obama alichokitaja kuwa ni "aina mpya ya ushirikiano" baina ya Marekani na China. Viongozi hao wawili walifanya mazungumzo ya muda mrefu ya kufahamiana katika eneo la mapumziko la Sunnylands, jimboni California. Obama na Xi hawakutoa taarifa zozote hadharani au katika mkutano wa pamoja na waandishi habari hapo jana, lakini Rais wa Marekani alisema Ijumaa jioni kuwa nchi hizo mbili zilikuwa na sehemu nyingi ambazo zilihitaji ushirikiano,licha ya kukikiri oia kwamba kuna masuala yenye utata, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya mtandaoni na masuala ya biashara. Ikulu ya Marekani imesema marais hao wawili wamekubaliana kushirikiana katika kupunguza utowaji wa gesi chafu ili kutatua suala la mabadiliko ya tabia nchi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO