Sunday, June 09, 2013

OMAR BASHIR AAMURU KUFUNGWA MABOMBA YA MAFUTA YA JIRANI ZAO

Rais wa Sudan Kaskazini Omar el Bashir ameamuru leo Jumapili, kufungwa kwa mabomba yanayosafirisha mafuta kutoka Sudan Kusini hadi bandari ya Port Sudan iliyoko kwenye Bahari Nyekundu, Kwa muda mrefu bandari hiyo inayomilikiwa na serikali ya Khartoum, imekuwa ikitumiwa na Sudan Kusini kusafirisha mafuta yake kwenye masoko ya nchi za kigeni.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Khartoum Ahmed Osama sababu za amri hiyo ya rais zinaelezwa kuwa ni msaada wa kijeshi ambao serikali ya Sudan Kusini inawapatia waasi wanaopigana kuiangusha serikali ya Khartoum. Uasi unaofanyika Kordofan Kusini unaungwa mkono kwa dhati na serikali ya Sudan Kusini ameeleza msemaji huyo wa serikali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO