Rais mpya wa Iran ameapa kuleta mabadiliko yanayotakiwa na wapiga kura baada ya miaka minane ya utawala wa kihafidhina. Hassan Rouhani pia amependekeza kufuata njia ya kuhusiana na mataifa mengine ya dunia. Rouhani ameeleza kuchaguliwa kwake kuwa ni enzi mpya na kusema atafuata njia ya wastani na haki, na kuielekeza nchi hiyo mbali na misimamo mikali. Rouhani ametoa matamshi hayo katika mkutano wake wa kwanza na waandishi habari tangu kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi na pia ameeleza haja ya kufanyakazi kuelekea uhusiano mzuri na jumuiya ya kimataifa. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 64 anatarajiwa kuchukua madaraka kutoka rais Mahmoud Ahmedinejad mapema mwezi wa August, na amesema amepata mamlaka maalum kutoka kwa wapiga kura kufanya mageuzi. Uchaguzi huo uliofanyika siku ya Ijumaa umeshuhudia akishinda asilimia 50 ya kura , ambapo watu waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 73.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO