Sunday, June 16, 2013

RAIS WA MISRI AKATA MAHUSIANO NA SYRIA

Rais Mohammad Morsi wa Misri amesema amekata uhusiano wa kidiplomasia na Syria na ameamuru ubalozi wa taifa hilo mjini Cairo ufungwe. Katika hotuba yake aliyoitoa jana katika mkutano wa viongozi wa kidini wa waislamu wa madhehebu ya Sunni mjini Cairo, Morsi amesema vilevile ametaka Waislamu wa Shia, wanaounda kundi la Hezbollah la Lebanon, kuondoka nchini Syria. Kiongozi huyo aliongeza kwa kusisitiza hakuna nafasi ya kundi hilo nchini Syria huku akiunga mkono marufuku ya kuruka ndege katika anga ya Syria. Wanadiplomasia wa mataifa ya magharibi ijumaa walisema Marekani inaangalia uwezekano wa kuweka marufuku ya kuruka ndege katika anga ya Syria ingawa ikulu ya taifa hilo baadae ilikanusha na kusema taifa hilo halina mpango huo. Urusi kama mshirika wa karibu wa Assad na mpinzani wa hatua yoyote ya kuingia kijeshi nchini Syria imesema jaribio la kuweka marufuku hiyo kwa kutumia ndege za kivita aina ya F16 na makombora ya Patroiti kutoka Jordan itakuwa sio halali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO