Sunday, June 16, 2013

SUDAN KUSINI YAKANUSHA KUSHAMBULIA MABOMBA YA MAFUTA

Jeshi la Sudan Kusini linakanusha madai ya Sudan kuwa imehusika na uharibifu na upasuaji wa mabomba yake ya mafuta katika eneo linalozozaniwa katika jimbo  la Abyei. Naibu msemani wa majeshi ya Sudan Kusini Malaak Ayuen ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa walisikia kupasuka kwa bomba la mafuta la Khartoum kupitia vyombo vya habari. Jeshi la Sudan linasema kuwa bomba la Khartoum liliharibiwa na waasi wa Sudan Kusini wa SPLM-N baada ya jeshi lake kuwapa msaada na mbinu za kufanya hivyo.
Matukio haya ya hivi punde yanakuja siku mbili baada ya Wizara ya mafuta nchini Sudan kutangaza mapema juma hili kufunga rasmi mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka nchini Sudan Kusini kuzuia mafuta yake kusafirishwa kwa mataifa mengine. Khartoum inasema kuwa hatua hiyo itadumu kwa siku sitini zijazo baada ya kuituhumu Juba kuwafadhili waasi wa SPM-N wanaopigana na majeshi ya serikali katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile. Mapema juma hili serikali ya Sudan ilitangaza kusitisha uhusiano wa kiusalama na kiuchumi na jirani yake Sudan Kusini kutokana na madai hayo ya kuwaunga mkono waasi tuhma ambazo Juba wamepinga.
Khartoum inasema kuwa uhusiano wake na Juba bado utasalia kuwa mzuri ikiwa  Sudan Kusini itaacha kuwaunga mkono waasi kwa kuwapa fedha na silaha, madai ambayo wamesema wamethibitisha kuwa Juba inahusika. Serikali ya Sudan Kusini inayoongozwa na rais Salva Kiir imeendela kukanusha madai hayop na kuwaomba raia wake kuendelea na maisha yao ya kawaida. Kiir ameimbia Khartoum kuwa hatua yao ya kufunga mabomba hizo hazitaathiri  uchumi wao na raia wake hawatakufa njaa kwa kile alichokisema kuwa raia wake wamekuwa wakiishi bila ya kutegemea mafuta.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO