Saturday, June 22, 2013

SHUGHULI ZA UOKOZI MAFURIKO INDIA ZAENDELEA

Shughuli ya kuwaokoa maelfu ya watu waliokwama kaskazini mashariki mwa India kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi inaendelea kufanyika nchini humo.Waziri wa mambo ya nje  Sushil Kumar Shinde amesema kiasi ya watu 30,000 tayari wameshahamishwa kutoka maeneo mbali mbali ya jimbo la milimani la Himachal Pradesh na kwamba maelfu ya wengine bado wamekwama.Shinde aliyasema hayo baada ya kulizuru eneo hilo kwa ndege. Afisa wa kushughulikia majanga kutoka mji mkuu wa jimbo hilo Dehradun amesema kuwa itachukua kipindi cha hadi wiki moja kuwaokoa watu hao takriban 30,000. Kundi la watalii 17 limehamishwa kwa ndege kutoka eneo la Dharasu huku kundi la mahujaji kiasi ya 1,000 wameonekana katika eneo kati ya Kedarnath na Gaurikund.Jumla ya miili 556 imepatikana chini ya vifusi vya majengo yaliyopromoka kutokana na maporomoko ya ardhi na inahofiwa kuwa miili zaidi imekwama chini ya vifusi hivyo.Jeshi la nchi hiyo,polisi na maafisa wa jimbo hilo wanashiriki katika shughuli hiyo ya uokozi na kutoa misaada ya dharura.Karibu helikopta 32 zinatumika katika shughuli hiyo. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO