Saturday, June 22, 2013

RAIS WA BRAZIL KUFANYA MAGEUZI YA SERA

Rais wa Brazil Dilma Rousseff amewasilisha kwa taifa hilo mageuzi kadhaa atakayotekeleza huku idadi ya waandamanaji wanaopinga ufisadi na sera za kiuchumi za nchi hiyo ikiongezeka.Rouseff amesema atawahimiza magavana wa majimbo na maafisa wa mabaraza ya miji kujadili masuala hayo na wawakilishi wa makundi yanayoandamana pamoja na vyama vya wafanyakazi kwa kuanzia na suala la usafiri wa umma.Pia amesema faida inayotokana na mafuta ya nchi hiyo, itatumika katika sekta ya elimu na maelfu ya madaktari wataletwa kutoka nchi za kigeni kuimarisha sekta ya afya.Rais huyo ametaka kukomeshwa kwa maandamano ambayo yameambatana na machafuko na kusema kuwa anawasikia wanaoandamana kwa amani kwani inadhihirisha udhabiti wa demokrasia lakini akasisistiza kuwa maafisa wa usalama watadumisha amani na hawataruhusu vitendo vya uporaji kwani vinalifedhehesha taifa hilo la Brazil.Maandamano yalizuka mjini Sao Paolo wiki iliyopita kupinga nyongeza ya nauli ya usafiri wa umma lakini yamejumuisha  sasa malalamiko ya  ufisadi na sera za matumizi ya fedha za umma.Inakisiwa watu milioni moja hapo jana walishiriki katika maandamano takriban katika miji kumi kote Brazil.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO