Wapiganaji wa Kitaliban wamesifu kufunguliwa ofisi yao nchini Qatar,wakiitaja hatua hiyo kama ni ushahidi wa mafanikio yao vitani lakini wameapa kuendelea na mapigano hadi pale vikosi vyote vya Marekani vitakapoondoka Afghanistan.Kufunguliwa ofisi hiyo nchini Qatar kumeonekana kama ni hatua ya kwanza kuelekea makubaliano ya amani wakati jeshi la Nato linaloongozwa na Marekani likiondoka kabisa mwishoni mwa mwaka ujao,lakini serikali ya Afghanistan imewashutumu waasi kwa kuweka serikali yao uhamishoni.Marekani imesisitiza kwamba ofisi hiyo isichukuliwe kama ni ubalozi wa Taliban walioondolewa madarakani mwaka 2001.Hapo jana msemaji wa serikali ya Afghanistan alisema lakini rais Karzai yuko tayari kushiriki mazungumzo ya amani na wataliban ikiwa kundi hilo litaondowa bendera na maandishi katika ofisi hiyo ya mjini Doha yanayoashiria ni ofisi ya kisiasa ya kundi hilo la Taliban.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO