Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu utiwaji mbaroni holela na matukio kadhaa ya mateso yanayojiri nchini Libya tangu kupinduliwa madarakani dikteta wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilitoa taarifa likieleza kuwa maelfu ya watu wametiwa nguvuni nje ya mamlaka ya serikali na kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria. Taarifa hiyo ilipasishwa jana na nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama.
Taarifa ya Baraza la Usalama pia imewataka viongozi wa Libya kuchunguza ukiukaji wote wa haki za binadamu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote wenye hatia.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO