Saturday, June 08, 2013

UFARANSA YAWAHOFIA WAASI WA SYRIA KWA ULAYA

Ufaransa ambayo ni moja ya nchi zinazounga mkono makundi ya waasi dhidi ya serikali ya Syria, imetangaza wasiwasi iliyonayo kutokana na kile ilichosema ni uwezekano wa kurejea kwa waasi hao barani Ulaya. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Manuel Valls, amefichua kuwa, tangu tarehe 15 Machi mwaka 2011 baada ya kuanza machafuko nchini Syria, zaidi ya raia wa nchi za Ulaya wapatao 600 wakiwamo Wafaransa 120 waliwasili nchini Syria na kujiunga na makundi ya waasi katika vita dhidi ya serikali ya Damascus na kwamba, hadi sasa kuna Wafaransa 40 ambao bado wako nchini humo. Manuel ameyasema hayo katika kikao cha kukabiliana na waasi barani Ulaya, kilichohudhuriwa na viongozi wa Ulaya huko nchini Luxembourg na kusisitiza juu ya udharura wa umoja huo kupanga mikakati ya kukabiliana na vitisho vya vijana wa nchi hizo wanaopigana nchini Syria. Amesisitiza kuwa, suala la kusikitisha ni kwamba, wengi wa vijana hao wamejiunga na makundi ya waasi ya Al-Qaida na Jabhat Nasra.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO