Saturday, June 08, 2013

WAZAYUNI WAFANYA NJAMA KUIGAWA SUDAN

Waziri wa Utamaduni na Habari wa Sudan, ameyataja mashambulizi ya makundi ya waasi nchini humo, kuwa yanayofanyika kwa njama za Wazayuni kwa minajili ya kuutokomeza umoja wa kitaifa na kuigawa nchi. Ahmad Bilal Othman ameyasema hayo kupitia redio ya Sudan na kufafanua kuwa, mashambulizi ya waasi nchini humo, yanafanyika kwa njama kamili za Wazayuni kwa lengo la kuharibu umoja na mshikamano, kuvuruga usalama na uthabiti wa Sudan, huku lengo kuu likiwa ni kuigawa nchi hiyo. Amesisitizia juu ya umuhimu wa kukabiliana na njama hizo za Israel dhidi ya Sudan. Hii ni katika hali ambayo kuna uwezekano serikali ya Khartoum ikakataa kufanya mazungumzo na waasi, baada ya waasi hao kutekeleza jinai mbalimbali dhidi ya wakazi wa Kordofan na Blue Nile katika siku za hivi karibuni.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO