Utawala wa Kizayuni wa Israel unatoa huduma za tiba kwa wapiganaji wa makundi ya waasi nchini Syria. Taarifa zinasema kuwa, mamia ya waasi hao ambao wamejeruhiwa kwenye mapigano dhidi ya majeshi ya Syria wanahamishiwa kwenye hospitali za Israel kwa minajili ya kupata huduma za tiba. Taarifa hizo zinasema kuwa, tokea mwezi Februari mwaka huu, madaktari na wafanyakazi wa hospitali za Israel wamepewa amri na makamanada wa jeshi la utawala huo kutoa huduma kwa majeruhi wanaopelekwa kwenye hospitali za utawala huo ghasibu. Hii ni katika hali ambayo, uingiliaji wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, pamoja na nchi za eneo kama vile Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye mgogoro wa Syria, umesababisha mgogoro wa nchi hiyo kushadidi na kuwa tata zaidi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO