Papa Francis 1, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameonana na ujumbe wa bunge la Ufaransa na kuzungumzia hatua ya bunge hilo kupitisha sheria inayoruhusu ndoa za watu wanaolawitiana. Katika mazungumzo aliyofanya na wabunge na maseneta wa Ufaransa huko mjini Vatican, pasina kubainisha waziwazi, Papa Francis amewataka wabunge na maseneta hao wa Ufaransa kufuta baadhi ya sheria ikiwemo ya watu wanaolawitiana ili kuinua nafasi ya sifa za fadhila, shakhsia na heshima ya utu. Huku akiashiria kwamba Ufaransa ni taifa linaloangaliwa na ulimwengu, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema miongoni mwa majukumu ya wabunge ni kuwafanya wananchi wawe na hali bora na vielvile kuchunguza kisheria na kitaalamu miswaada, kuipitisha, kuirekebisha na baadhi ya wakati kuifuta kabisa miswaada hiyo.
Licha ya upinzani wa harakati za kidini na za wananchi pamoja na maandamano makubwa ya upinzani yaliyofanywa katika miji mbalimbali ya Ufaransa, tarehe 23 ya mwezi Aprili mwaka huu bunge la nchi hiyo lilipitisha sheria inyoruhusu ndoa za watu wanaolawitiana.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO