Tuesday, July 02, 2013

AFUNGWA KWA KUIVUNJIA HESHIMA QUR AN

Mahakama ya Strasbourg nchini Ufaransa imemuhukumu adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela na faini ya euro 1,000 raia wa nchi hiyo aliyepatikana na hatia ya kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, Qurani Tukufu.
Mahakama hiyo imeeleza kuwa, mhalifu huyo alikuwa akitafutwa na vyombo vya sheria kwa kosa la kuteketeza moto na kukivunjia heshima kitabu hicho kitakatifu.
Vitendo vya chuki na uadui dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu vimekuwa vikishamiri kila uchao nchini Ufaransa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kushambuliwa wanawake wanaovaa hijabu ya Kiislamu katika eneo la Val-d'Oise kaskazini mwa Ufaransa.
Hivi karibuni Baraza la Utamaduni la Waislamu nchini Ufaransa CFCM lilitangaza kuwa, kuanza mwaka huu wa 2013, zaidi ya misikiti 10 imeshambuliwa na kuvunjiwa heshima na Wafaransa wenye chuki na uadui dhidi ya Uislamu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO