Gazeti la La Libre linalochapishwa nchini Ubelgiji limeandika kuwa, harakati ya Hizbullah nchini Lebanon licha ya kuwa na nguvu kubwa kuliko jeshi la Lebanon, inazishughulisha na kuziumiza mno fikra za makamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel. Toleo la jana Jumatatu la gazeti hilo limeandika kuwa, Brigedia Jenerali mstaafu Joshua Ben Anat, kamanda wa zamani wa vikosi vya dhiba vya jeshi la Israel amesema kuwa, harakati ya Hizbullah ina uwezo wa kushambulia kwa makombora ya masafa ya karibu, wastani na ya mbali, miji mbalimbali ya utawala huo ukiwemo Tel Aviv.
Gazeti la La Libre limeeleza kuwa, harakati ya Hizbullah inayoongozwa na Sayyid Hassan Nasrullah imekuwa hatari kwa utawala wa Israel na kwa minajili hiyo nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinafanya juhudi za kuliweka tawi la kijeshi la harakati ya Hizbullah kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.
Gazeti hilo limeelezea pigo kubwa lililotolewa na wapiganaji wa Hizbullah dhidi ya majeshi ya Israel katika vita vya siku 33 mwaka 2006, na kusisitiza kuwa, majeshi ya Israel hayana hamu ya kuivamia tena ardhi ya kusini mwa Lebanon baada ya kupigwa na kufukuzwa kwa madhila makubwa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO