Wednesday, July 03, 2013

AHMED NEJAD AISIFU GECF

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Jumuiya ya nchi zinazozalisha gesi kwa wingi duniani (GECF) inazidi kustawi na kuwa taasisi yenye nguvu duniani. Rais Ahmadinejad ameyasema hayo leo katika siku ya pili na ya mwisho ya safari yake mjini Moscow, Russia na kusisitiza kuwa, Iran ina mpango kabambe wa kuimarisha jumuiya na mwenendo wa uongozi wa soko la gesi duniani. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefafanua kuwa, sehemu kubwa ya akiba ya gesi duniani inapatikana katika nchi za Iran na Russia na kwamba, ushirikiano wa nchi hizi mbili ndani ya jumuiya ya GECF utasaidia kuimarisha jumuiya hiyo na kuifanya ipige hatua kubwa zaidi za kusonga mbele. Akiashiria ushirikiano chanya na mzuri uliopo kati ya wanachama wa jumuiya hiyo na kufanyika kwa mafanikio kikao cha viongozi wa jumuiya hiyo huko mjini Moscow, Rais Ahmadinejad amekitaja kikao hicho cha siku mbili kuwa kimefanyika kwa ufanisi mkubwa na kimekurubisha pamoja mitazamo ya nchi wanachama kuelekea kwenye taasisi yenye taathira chanya kimataifa. Aidha rais huyo ameashiria uhusiano mzuri kati ya Iran na Russia na kusisitiza kuwa, kwa kuzingatia kwamba nchi hizi mbili ziko kwenye kambi moja, basi zinatakiwa kupigania usawa na kujitegemea sambamba na kupambana na kupenda kujitanua wakoloni wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO