Tuesday, July 16, 2013

VURUGU ZAANZA TENA MISRI

Mamia ya wafuasi wa kiongozi aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi wamepambana na vikosi vya usalama katikati mwa mji wa Cairo na kuwafyatulia waandamanaji hao gesi ya kutoa machozi. Mapigano hayo yanajiri muda mfupi baada ya mjumbe mkuu wa Marekani William Burns kutoa wito kwa vikosi vya usalama kujizuia kwa kiwango kikubwa katika kukabiliana na maandamano hayo.Makabiliano yalifanyika baada ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayezuru Misri, kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutuliza ghasia wakati wakijizuia kufanya mauaji yoyote.
Burns alikutana na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na majeshi. Lakini chama cha Muslim Brotherhood kimesema haikina nia ya kukutana na waziri huyo. Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi nchini, mjumbe huyo, William Burns, amesema Misri imepewa nafasi ya pili kufuatia kupinduliwa na jeshi Mohammed Morsi. Alikutana na serikali inayoungwa mkono na jeshi nchini lakini Muslim Brotherhood, inasema haina mpango wa kukutana naye. Naibu rais wa tawi la kisiasa la chama cha Morsi, Muslim Brotherhood,Essam el-Erian, ametoa wito wa utulivu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO