Bunge la Ulaya leo limeitaka serikali ya Marekani itoe ufafanuzi wa haraka kuhusu madai kwamba Marekani inazifanyia upelelezi ofisi za Umoja wa Ulaya na imeonya kwamba kashfa hiyo ya ujasusi inaweza kuathiri uhusiano wa kidiplomasia. Katika azimio lililopitishwa kwa kauli moja na bunge hilo lenye makao yake mjini Strassbourg, bunge hilo limelaani kupelelezwa kwa mabalozi wa Umoja wa Ulaya na kuonya juu ya uwezekano wa kuwepo kwa taathira katika uhusiano kati ya Marekani na Ulaya.
Hata hivyo wabunge hao wamekataa kipengee cha wabunge wa sera za mrengo wa shoto na wale wa sera kali za mrengo wa shoto kufutwa kwa mazungumzo kuhusu makubaliano makubwa ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani yanayotazamiwa kuanza Jumatatu ijayo. Hoja nyengine iliyokataliwa ni kwa mataifa ya Ulaya kumpa hifadhi mfanyakazi wa zamani wa shirika la usalama la taifa la Marekani, Edward Snowden, aliyevujisha taarifa za kutegeshwa kwa balozi na taasisi za Umoja wa Ulaya kulikofanywa na Marekani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO