Umoja wa Afrika yumkini ukasitisha uwanachama wa Misri katika umoja huo baada ya jeshi la nchi hiyo kuisitisha katiba ya nchi hiyo na kumpindua rais aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia. Afisa mwandamizi wa umoja huo aliyekataa kutajwa jina lake amesema leo hii wajumbe wa kamati ya baraza la amani na usalama la umoja huo watakutana kesho Ijumaa na yumkini wakachukuwa hatua kama ilivyo kawaida kwa umoja huo dhidi ya aina yoyote ile ya kuvuruga utawala wa kikatiba kunakofanywa na nchi wanachama wake. Amesema imani iliyopo ni kwamba nadharia hiyo itatumika ambayo ni kusitishwa kwa uwanachama wa nchi yoyote ile ambamo mabadiliko ya utawala kinyume na katiba yamefanyika.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO