Monday, July 15, 2013

ISRAEL YAWAFUNGA JELA VIONGOZI WA PALESTINA

Utawala wa Kizayuni wa Israel umewahukumu Khalid abu A'rafa waziri wa zamani aliyekuwa akishughulikia masuala ya Baitul Muqaddas katika serikali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina na Mahmoud Twautwah mbunge wa Bunge la Palestina kifungo cha miaka miwili na nusu jela kila mmoja. Shakhsia hao wawili wa Palestina walitiwa mbaroni na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel tarehe 23 Januari 2012. Hadi sasa wabunge wasiopungua 12 kutoka chama cha Hamas, bado wanashikiliwa kwenye jela za utawala huo. Izzat ar Rashaq mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amelaani vikali hukumu hiyo ya kidhuluma na kusisitiza kuwa, mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu na wapenda uhuru duniani wanapaswa kuchukua hatua ya kusaidia kuachiliwa huru mateka wa Kipalestina wanaoendelea na mgomo wa chakula pamoja na wengine ambao ni wagonjwa wanaoendelea kushikiliwa kwenye jela za Israel. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi sasa kuna Wapalestina wasiopungua elfu tano wanaondelea kushikiliwa kwenye jela za utawala wa Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO