Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limefanikiwa kuwakomboa raia kadhaa wa nchi hiyo, waliokuwa wametekwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram. Jishi hilo limetangaza kuwa, raia hao waliokuwa wakishikiliwa na kundi hilo huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, wamekombolewa kufuatia oparesheni iliyofanikiwa baada ya kuwaua wapiganaji wa kundi hilo. Aidha jeshi hilo limethibitisha kujiri mapigano makali na wapiganaji wa Boko Haram katika eneo la Bulabulin Nganaram mjini Maiduguri. Wakati huo huo, jeshi la Nigeria, limetangaza kugunduliwa kaburi la umati mjini Maiduguri na kwamba, waliouawa ni raia wa kawaida. Mapigano kati ya jeshi na kundi la Boko Haram, yanajiri katika hali ambayo, mwanzoni mwa mwezi huu wa Ramadhani pande mbili zilikubaliana kusimamisha mapigano kati yao kwa mnasaba wa kuwadia mwezi huu mtukufu. Mkuu wa tume ya kufanya mazungumzo na Boko Haram, Bwana Tanimu Turaki amewaambia waandishi wa habari kuwa, makubaliano hayo ya usitishaji mapigano kati ya serikali na kundi hilo, yalifikiwa baada ya kujiri mazungumzo ya muda mrefu kati ya pande hizo mbili hasimu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO