Thursday, July 04, 2013

JAJI ADLY AL-MANSOUR AWA RAIS WA MPITO WA MISRI

Jaji Mkuu Adly al-Mansour Kulingana na mpango wa jeshi jaji huyo mkuu ameapishwa leo Alhamisi na kuchukua nafasi ya kuongoza serikali ya mpito itakayoundwa. Hatua ya kupishwa kwa jaji imekuja baada ya Jeshi nchini Misri kumpindua na kumkamata Rais wa nchi hiyo, Mohamed Morsi jana kufuatia vurugu za juma zima na maandamano yaliyokuwa yakishinikiza Rais huyo kujiuzulu.
Akiapishwa mahakama ya juu ya katiba, Adly al-Mansour ameahidi katiba na utawala wa sheria na ataongoza serikali ya mpito kwa kulinda matakwa na vipaumbele vya raia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema kuwa hatua ya jeshi la Misri kuingilia kati na kuuondoa utawala uliowekwa madarakani kwa njia za kidiplomasia si sahihi. Amema kuwa kitendo hicho kinarudisha nyuma jitihada za kukuza demokrasia nchini humo na ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na kufikiwa kwa muafaka wa kisiasa kwa ajili ya mustakabali wa baadaye wa Misri.
Guido Westerwelle amebainisha kuwa mapinduzi hayo ni hatari kwa nchini ya Misri na kipindi cha mpito kuelekea demokrasia ya kweli kimevurugwa na kuharibiwa vibaya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO