Thursday, July 04, 2013

CHINA NA IRAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA USALAMA

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Mostafa Mohammad-Najjar amesisitiza juu ya kuimarishwa uhusiano wa kiusalama baina ya Tehran na Beijing. Ameongeza kuwa nchi hizi mbili zinalipa umuhimu mkubwa suala la usalama na utulivu katika eneo.
Mohammad-Najjar ameyasema hayo mapema leo baada ya kuwasili katika mji mkuu wa China, Beijing kwa ziara rasmi ya siku nne. Ameongeza kuwa Iran na China zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kiusalama.
Amesema katika ziara hiyo mkataba muhimu wa ushirikiano wa kiusalama utatiwa saini baina yake na Waziri wa Usalama wa Umma wa China Guo Shengkun.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO