Mustapha Barghouthi mmoja kati ya viongozi wa mapambano wa Palestina amejeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na askari wa Israel.
Barghouthi alijeruhiwa jana katika shambulizi lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayauni dhidi ya maandamano ya Wapalestina huko katikati ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwenye mji wa Beitin. Kiongozi huyo wa muqawamah wa Palestina amesema, askari wa Israel pia wamewajeruhi makumi ya Wapalestina wengine waliotoka katika miji ya Jenin, al Khalil, Nablus, Ramallah na Tulkarem kwenye tukio hilo. Barghouth amesema, matumizi ya mabavu dhidi ya maandamano ya amani hayatawazuia Wapalestina kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zao.
Hatua ya Israel ya kuendelea kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina inazozikalia kwa amabavu imekuwa kikwazo kikuu cha kupatikana amani Mashariki ya Kati. Umoja wa Mataifa na nchi nyingi duniani zinasema kwamba, vitongoji hivyo vya Israel si halala kwa kwamba vinajengwa katika ardhi za Palestina zilizoporwa katika vita vya mwaka 1967 na Mkataba wa Geneva unazuia kujenga katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO