Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu elfu tano wanakufa kila mwezi katika vita vya Syria, ambavyo vimesababisha mgogoro mkubwa wa wakimbizi tangu ule uliofuatia mauwaji ya kimbari ya Rwanda mwaka wa 1994. Maafisa kadhaa wakuu wa Umoja wa Mataifa wamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililogawanyika kuchukua hatua dhabiti za kukabiliana na mgogoro huo uliodumu miaka miwili, na ambao umeaminika kusababisha vifo vya watu laki moja. Kamishena wa Umoja wa Mataifa anayesimamia masuala ya wakimbizi Antonio Guteress amesema karibu watu milioni 1.8 sasa wamejisajili na Umoja wa Mataifa katika nchi jirani na Syria na karibu watu 6,000 wanakimbia kila siku. Amesema nchi za Lebanon, Iraq, Jordan na nyingine ambazo zinawahifadhi wakimbizi wa Syria zinaokoa mamia kwa maelfu ya maisha.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO