Waendesha mashitaka nchini Misri watachunguza madai kuhusu rais aliyeondolewa madarakani, Muhammed Mursi kwamba alitoroka jela wakati wa vuguvugu la mageuzi la mwaka 2011, akisaidiwa na kundi la wanamgambo la Wapalestina la Hamas. Mwendesha mashitaka mkuu wa Misri, Hesham Barakat amepokea ushahidi kutoka kwenye mahakama moja ya Ismailia, utakaotumika kama msingi wa uchunguzi utakaofanywa na waendesha mashitaka wa serikali kwamba Mursi na viongozi wengine zaidi ya 30 wa chama cha Udugu wa Kiislamu, walitoroka jela. Wakati huo huo wafuasi wa Mursi na wale wanaompinga wanatarajiwa kufanya maandamano baadae leo mjini Cairo. Hali hiyo inazusha wasiwasi wa kutokea ghasia kutokana na jeshi kumpindua kiongozi huyo. Wafuasi wa Mursi wataandamana mashariki mwa Cairo, huku wanaompinga wakiandamana kwenye uwanja wa Tahrir.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO