Siku moja baada ya jeshi la Misri kutoa waranti ya kukamatwa kiongozi mkuu wa harakati ya Ikhwanul Muslimin, Mohammad Badie, harakati hiyo imetishia kutangaza jihadi dhidi ya jeshi iwapo kiongozi huyo atatiwa nguvuni. Maafisa waandamizi wa harakati hiyo wamesema Badie si mwanasiasa na kwamba hafai kuhusishwa na masuala ya kisiasa. Huku hayo yakijiri, Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito ya Misri, Hazem al-Beblawi amesema waranti dhidi ya Badie umevuruga mipango yake ya kuunda serikali mpya. Amesema fursa iliyokuwepo ya kuwashawishi wafuasi wa Ikhwan kujiunga na serikali sasa imetoweka kabisa. Tayari Ikhwanul Muslimin wamesema hawatokubali kushikilia nyadhifa zozote kwenye serikali na kwamba wanachotaka ni Dk Muhammad Mursi kurudishiwa wadhifa wake wa urais. Waziri Mkuu amesema serikali mpya itakuwa tayari imeundwa ifikapo Jumapili ijayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO