Saturday, July 13, 2013

NJAMA ZA ISRAEL KUTAKA KUISHAMBULIA HIZBULLAH

Utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya manuva ya kijeshi yaliyokwenda sambamba na kutoa mafunzo na mbinu kwa wanajeshi wa Israel za kuwashambulia wanamapambano wa Hizbullah kusini mwa Lebanon. Manuva hayo ya kijeshi ya Israel yamefanyika katika kambi ya kijeshi iliyoko karibu na mji wa Haifa. Kambi hiyo ilijengwa mwaka 2006, baada ya majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kusalimu amri mbele ya wanamapambano wa Hizbullah kusini mwa Lebanon. Mara kwa mara majeshi ya Israel yamekuwa wakikiuka sheria za kimataifa kwa kuingia ndani ya ardhi ya Lebanon kupitia angani, ardhini na majini. Vitendo hivyo vya Israel vinakinzana na azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililotolewa baada ya kumalizika vita vya siku 33 kati ya utawala wa Israel na wanamgambo wa Hizbullah. Azimio hilo, liliutaka utawala wa Israel uheshimu haki ya kujitawala ya ardhi yote ya Lebanon.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO