Mwanaharakati wa ndoa za watu wa jinsia moja na mwandishi wa habari wa Cameroon, Eric Lembembe ameuawa mjini Yaounde na mwili wake kutelekezwa, mashirika ya kutetea haki za binadamu yamedhibitisha. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na muungano wa mashirika hayo, imesema kuwa shingo na miguu ya mwanaharakati huyo ilikuwa imevunjika huku maeneo ya mkononi na usoni akiwajumuisha amechomwa na pasi. Mpaka sasa sababu ya mauaji yake hazijajulikana licha ya hivi karibuni kabla ya kifo chake kudai kuwa amekuwa akipokea ujumbe wa vitisho toka kwa watu wasiofahamika. Suala la ushoga na ndoa za watu wa jinsia moja linepigwa marufuku nchini Cameroon na yeyote ambaye anapatikana na hatia ya kitenda kosa hilo anahukumiwa.
Mmoja wa viongozi wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Cameroon, Neela Ghoshal amesema polisi hawapaswi kufumbia macho mauaji hayo kwakuwa hata Lembembe mwenyewe alishawahi kuandika maelezo polisi kueleza kupokea vitisho toka kwa watu wasiofahamika. Suala la ndoa za watu wa jinsia moja limepigwa marufuku katika mataifa mengi ya bara la Afrika ambapo wanaopatikana na hatia ya kutenda kosa hilo katika baadhi ya nchi, adhabu yake ni kunyongwa. Mataifa ya magharibi yamejikuta yakiingia kwenye mzozo na mataifa ya Afrika kutokana na baadhi Yao kutishia kusitisha misaada iwapo nchi zao hazitakubakiana na kuruhusu ndoa za watu wa jinsia moja. Ukanda wa Afrika Mashariki ni moja ya maeneo ambayo nchi wanachama haziruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO