Saturday, July 13, 2013

WAANDAMANAJI WAENDELEA KUDAI KURUDISHWA MADARAKANI RAIS MURSI

Maelfu kwa maelfu ya Wamisri wameandamana barabarani kutaka kurejeshwa madarakani kwa Mohammed Morsi.Kiongozi huyo wa chama cha Udugu wa kiislamu aliekuwa Rais wa Misri, alitolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.Wakati huo huo, Ujerumani na Marekani zimetoa  mwito wa kuachiwa kwa mwanasiasa huyo aliewekwa mahabusu na jeshi.Morsi hajaonekana, tokea alipoangushwa na  kukamatwa na wanajeshi.Chama chake cha Udugu wa kiislamu kinakataa kushiriki katika serikali ya kipindi cha mpito inayodhibitiwa na jeshi.Wafuasi wa Morsi wamesema wataziendeleza harakati zao hadi hapo Morsi atakaporejeshwa madarakani. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO