Tuesday, July 16, 2013

RAIA WA UFARANSA AUAWA MALI

Mwili uliopatikana Kaskazini mwa Mali , umethibitishwa kuwa wa mwanamume aliyekamatwa na wapiganaji wa kiisilamu mwaka 2011. Hii ni kwa mujibu wa duru kutoka ofisi ya rais.Tawi la kundi la kigiaid la Al-Qaeda, Kaskazini mwa Afrika, limesema kuwa lilimuua mwanajiolojia Philippe Verdon katika kulipiza kisasi hatua ya jeshi la Ufaransa kusaidia Mali. Bwana Verdon na mwanamume mwengine raia wa Ufaransa, alikamatwa mjini Hombori kaskazini mwa nchi.
Alisemekana kuwa katika safari ya kibiashara alipotekwa nyara Novemba mwaka 2011. "kifo cha mwenzetu Philippe Verdon, kimethibitishwa rasmi,'' ilisema taarifa kutoka ofisi ya rais Francois Hollande.
"mwili wake utahamishwa hadi Ufaransa mara moja na kuwa uchunguzi utasaidia kubaini chanzo cha kifo chake.'' Ufaransa ilituma majeshi nchini Mali mwezi Januari, ikielezea hofu kuwa wapiganaji wa Al qaeeda huenda wakavamia mji mkuu Bamako. Kando la hilo, Bwana Verdon na raia wengine sita wa Ufaransa, wanazuiliwa na wanamgambo wa kiisilamu nchini humo. Kwenye mahojiano siku ya Jumapili, bwana Hollande alisema kuwa alikuwa anafanya kila awezalo kuwarejesha wale waliozuiliwa nyumbani haraka iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO