Mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani, Edward Snowden, amesema ataomba hifadhi ya kisiasa nchini Urusi, kwa sababu hawezi kwenda sehemu nyingine yoyote. Snowden leo alikutana na wanaharakati wa haki za binaadamu na wanasheria. Mwakilishi wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch, Tanya Lokshina, ameliambia shirika la habari la Interfax kwamba Snowden anataka kubakia Urusi. Msemaji wa uwanja wa ndege, Anna Zakharenkova, amesema kuwa watu 13 walihudhuria mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow. Aidha, Urusi imesema Snowden anaweza kubakia nchini humo iwapo ataacha kuvujisha siri sitakazoharibu sura ya Marekani. Kauli hiyo imetolewa leo na Ikulu ya Urusi, baada ya Snowden kusema ataomba hifadhi nchini Urusi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO