Wednesday, July 03, 2013

SUDAN YATAKA KUONDOLEWA VIKWAZO

Chama cha Kongresi ya Kitaifa cha Sudan kimeitaka jamii ya kimataifa ifanye juhudi za kufutiwa vikwazo nchi hiyo. Al-Haj Adam Youseff, Makamu Mwenyekiti wa chama cha National Congress Party (NCP) kinachotawala nchini Sudan ameitaka jamii ya kimataifa  iiondoleee vikwazo Sudan na hivyo kuisaidia katika uwanja wa ustawi na maendeleo. Kiongozi huyo mwandamizi wa chama tawala nchini Sudan amesema kuwa, licha ya kuweko mzingiro na njama za maadui za kuusambaratisha uchumi wa nchi hiyo, lakini katika kipindi cha miaka 24 iliyopita Khartoum  imeweza kupiga hatua muhimu za kimaendeleo. Makamu Mwenyekiti wa chama tawala nchini Sudan cha National Congress Party (NCP) ameyataka makundi yote ya kisiasa nchini humo kujiunga na hati ya makubaliano ya amani na hivyo kusaidia juhudi za kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO