Wednesday, July 03, 2013

WANANDOA WAHUKUMIWA KWA UJASUSI UJERUMANI

Mahakama ya Ujerumani imewakuta na hatia mtu mmoja na mkewe kwa kufanya upelelezi kwa niaba ya Urusi na kuwahukumu vifungo gerezani.
Watu hao walikamatwa hapo mwaka 2011 baada ya kuishi katika hali ya maisha isoeleweka nchini Ujerumani. Mahakama Kuu ya Jimbo la Stuttgart leo hii imewahukumu wana ndoa hao wanaoishi Ujerumani kutumikia vifungo gerezani baada ya kuwaona na hatia ya kuwa wapelelezi wa Urusi. Andreas Anschlag amehukumiwa kifungo cha miaka sita na nusu gerezani wakati mke wake Heidrun Anschlag amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na nusu gerezani. Wote wawili walikuwa wakiishi Ujerumani kwa kutumia paspoti bandia za Austria. Utambulisho wao halisi unajulikana na mahakama tu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO